Winga Muargentina Angel Di Maria amesema hajutii hata kidogo kuihama klabu ya Real Madrid na kutua Manchester United.
Di Maria ambaye alitua Manchester United kwa uhamisho wa rekodi wa karibia €70 na kuzua vita vya maneno kati yake na klabu ya Real Madrid akifanya mahojiano na Televisheni ya Ufaransa Telefoot amesema
``Sijuti kuhama Real Madrid,nimepata kila nilichokihitaji kama mchezaji ambacho ni mataji.Nimetwaa La Liga,Copa Del Rey na Ligi ya mabingwa"
``Nafurahia maisha Manchester japo soka la hapa siyo sawa na lile la La Liga"
Asema kuondoka United kunawezekana Siku za usoni
``Leo niko England lakini kuhama inawezekana kwani katika soka kuna kuhamahama kwingi leo unaweza ukawa hapa kesho pale!
0 comments:
Post a Comment