Shirikisho la soka Tanzania, TFF, limesema
linakaribisha wabunifu watakaobuni
mwonekano wa jezi mpya za timu ya taifa kwa
mechi za nyumbani na ugenini.
Hata hivyo sharti la ubunifu huo lazima
uzingatie rangi za bendera ya taifa ambazo ni
kijani, njano, nyeusi na bluu.
Wakati tangazo hili likitolewa na TFF, tayari
uongozi mpya chini ya rais wake Jamal
Malinzi umebadili jezi zinazotumiwa katika
mechi za timu ya taifa, Taifa Stars, kutoka zile
zilizozoeleka na mashabiki na Watanzania
wote hadi jezi mpya zinazolalamikiwa na
mashabiki wengi kuwa hazina mvuto na
hazionyeshi rangi halisi ya bendera ya taifa la
Tanzania.
Jezi mpya ya timu ya taifa ya Tanzania,
ambayo nayo inatakiwa kubadilishwa
TFF ilipoamua kutumia jezi mpya
zinazotumika sasa haikuwashirikisha
wabunifu wa mavazi kuhusu jezi mpya ya timu
ya taifa na badala yake ikaja na jezi ambayo
imekuwa ikilalamikiwa na mashabiki kuwa
haina mvuto na haiwakilishi rangi halisi za
bendera ya taifa, huenda ndio maana safari
hii wametoa tangazo hilo.
Mbunifu atakayeshinda atapata zawadi ya
shilingi milioni moja za Kitanzania sawa na
karibu dola mia saba za Kimarekani kwa
atakayebuni jezi ya kuchezea mechi za
nyumbani na vile vile mshindi atakayebuni jezi
za kuchezea mechi za ugenini naye atapata
kiasi kama hicho cha fedha.
Jezi ya sasa ina rangi ya samawati na bluu
nyeusi.
0 comments:
Post a Comment