728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, November 19, 2014

    DI MARIA HATIHATI KUIVAA ARSENAL JUMAPILI

    Winga wa klabu ya Manchester United Muargentina Angel Di Maria anasubiri vipimo vya X-ray ili kujua kama atakuwa miongoni mwa nyota wa klabu hiyo watakaoshuka katika dimba la Emirates kuwavaa wenyeji Arsenal jumapili hii baada ya kuumia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Argentina dhidi ya Ureno uliopigwa jana katika dimba la Old Trafford.

    Di Maria 26 alichezewa madhambi na Louis Nani nyota wa Manchester United aliyeko kwa mkopo katika klabu ya Sporting Lisbon na kulazimika kutolewa uwanjani dakika ya 61 ya mchezo huo ambao uliisha kwa Argentina kulala kwa goli 0-1.

    Akizungumza baada ya mchezo kumalizika winga huyo alisema jeraha lake hilo siyo kubwa sana ila kinachosubiriwa ni vipimo vya X-ray vitakavyofanywa leo ili kujua ukubwa/udogo wa tatizo.

    Ikiwa Di Maria atakosa mchezo huo wa jumapili hili litakuwa ni pigo jingine kwa klabu ya Manchester United baada ya mapema wiki hii kuwapoteza viongo wake wawili Delay Blind na Michael Carrick kutokana na majerahi lakini mlinda mlango David De Gea yeye ameripotiwa kuendelea vizuri baada ya kuteguka kidole katika mazoezi ya timu yake ya taifa ya Hispania ``La Roja"

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DI MARIA HATIHATI KUIVAA ARSENAL JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top