Klabu ya Chelsea imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifungwa Liverpool kwa magoli 2-1 katika mchezo ulioisha hivi punde katika dimba la Anfield.
Liverpool ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata goli la kuongoza dakika ya 9 tu ya mchezo baada ya kiungo wake Emre Can kupiga shuti kali lililombabatiza mlinzi wa Chelsea Garry Cahill na kutika wavuni.
Baada ya goli hilo Chelsea waliamka na kufanikiwa kusawazisha goli hilo kupitia kwa mlinzi Garry Cahill dakika ya 14 na kufanikiwa kupata goli la ushindi dakika ya 67 kupitia kwa mshambuliaji Diego Costa baada ya kazi nzuri toka mlinzi wa kushoto Cesar Azpilicueta.
Baada ya kichapo hicho Liverpool inajikita nafasi ya nane huku Chelsea ikiwa kileleni kwa pointi 29 pointi 7 dhidi ya klabu ya Southampton iliyoko nafasi ya pili.
0 comments:
Post a Comment