BOSI wa Ufundi wa Yanga, Marcio
Maximo, amesema anataka wachezaji
wapya wawili tu anaosema wakitua
klabuni hapo tu basi kazi imeisha na
ubingwa ataupata kiulaini kabisa, mmoja
atakuwa mzawa.
Maximo alisema baada ya kukifanyia
tathimini kikosi chake amegundua
kwamba amepungukiwa viungo wawili
wa kati ambao lazima anunue wapya
kwenye dirisha dogo la usajili linaloanza
wikiendi ijayo.
Alisema katika mapendekezo yake
anataka Kamati ya Usajili ya timu hiyo
iliyochini ya Mhandisi Isaac Chanji, Seif
Ahmed ‘Seif Magari’, Abdallah Bin Kleb
na Mussa Katabaro, kusaka kiungo mmoja
mzawa na mwingine wa kigeni huku
akigoma kutaja majina yao ingawa
Mwanaspoti lina taarifa za awali.
“Ukiangalia timu utaona kwamba hakuna
uwiano sawa kati ya viungo na
washambuliaji, sasa tuna washambuliaji
wengi kuliko viungo hiyo sio sawa sana,
tunahitaji kuongeza watu wawili
watakaotuongezea nguvu,” alisema
Maximo ambaye ameondoka nchini leo
sambamba na wachezaji Wabrazili
kwenda likizo ya siku 10.
“Nataka wachezaji wawili tu kwa sasa,
tayari nimeshawapa majina ya watu
ninaowataka, siwezi kukutajia ni nani na
nani, lakini tambua kwamba tayari
nimeshawasiliana nafikiri mpaka nikirudi
baada ya siku 10 naweza kuwakuta
hapa,”alisema Maximo.
Wakati Maximo akigoma kuwataja,
Mwanaspoti linafahamu kwamba endapo
Yanga itamkosa kiungo Jonas Mkude wa
Simba itahamishia rada kwa Shaban Nditi
wa Mtibwa Sugar.
0 comments:
Post a Comment