728x90 AdSpace

Monday, November 10, 2014

MSUVA:KUANZIA BENCHI RAHA SANA

WINGA mwenye kasi zaidi kwenye kikosi
cha Yanga, Simon Msuva, amesema
chachu ya kuifunga Mgambo JKT mabao
mawili juzi Jumamosi ni yeye kuanzia
benchi kwani alipata muda mzuri wa
kuwasoma wapinzani na kufahamu
mapungufu yao.
Msuva aliingia kipindi cha pili kwenye
mchezo huo akichukua nafasi ya Haruna
Niyonzima na kufanikiwa kufunga mabao
hayo na kuiwezesha Yanga kuchomoza na
ushindi wa mabao 2-0 mbele ya kikosi
cha wachezaji 10 wa Mgambo.
Winga huyo alisema licha ya kwamba
Yanga walifanikiwa kushinda, bado
wapinzani wao walionekana kuwa wazuri
na kuwapa changamoto kubwa.
“Nilipokuwa benchi nilifanikiwa
kuwasoma wapinzani, nilifahamu uzuri
wao na ubovu wao, hivyo nilivyoingia
kazi yangu haikuwa ngumu sana,”
alisema.
“Kocha pia alinipa maelekezo ya namna
ya kwenda kupenya kwenye ukuta wa
wapinzani wetu ambao walionekana
kuwa imara sana, haikuwa kazi rahisi
lakini nilijitahidi kupambana.”

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: MSUVA:KUANZIA BENCHI RAHA SANA Rating: 5 Reviewed By: Unknown