Mlinzi mahiri wa klabu ya Manchester City Mbelgiji Vincent Kompany amesema kamwe hawezi kuhamia klabu ya Arsenal hata kama atapewa donge nono la £60m pamoja na magari mawili ya kifahari aina ya Ferrari.
Kompany ametoa tamko hilo kupitia ukurasa wake twitter kufuatia shabiki maarufu wa klabu ya Arsenal bwana Piers Morgan kuandika katika ukurasa wake wa twitter kama kuna siku nyota huyo wa zamani wa Anderletch anaweza kuhamia Arsenal.
Majibizano hayo kwenye twitter yaliibuka baada ya Piers Morgan kukerwa na uzembe ulioonyeshwa na walinzi wa Arsenal hata kuruhusu kufungwa magoli matatu na kuufanya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Anderletch umalizike kwa magoli 3-3 licha ya Arsenal kuongoza 3-0 kwa kipindi kirefu cha mchezo.
Kompany akiwa ameguswa na maneno ya Morgan alisema
``Naiheshimu Arsenal kwa mambo yote,ukubwa na mafanikio yake lakini hawezi kushawishika kuhamia hata kwa £60m pamoja na magari mawili ya kifahari ya Ferrari"
0 comments:
Post a Comment