Klabu ya Real Madrid imeiambia klabu ya Manchester United kuwa haitampa mkataba wa kudumu nyota aliyeko klabuni hapo kwa mkopo Mmexico Javier Hernandez maarufu kama Chicharito.
Habari kutoka nchini Hispania zinadai klabu hiyo nyenye makazi yake katika dimba la Santiago Bernabeu haijaridhishwa na kiwango cha nyota huyo hivyo baada ya mtakaba wake wa mkopo kuisha mwezi mei atarejea Old trafford.
Chicharito alijiunga na Real Madrid mwezi wa tisa baada ya kuambiwa hayuko katika mipango ya kocha Louis Van Gaal hasa baada ya ujio wa mshambuliaji Mcolombia Radamel Falcao akitokea Monaco ya Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment