MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrisho Ngassa
amepata zali Afrika, baada ya kumaliza
kinara wa mabao kwenye Ligi ya
Mabingwa Afrika, licha ya klabu yake
kuaga mashindano hayo alfajiri kabisa.
Ngassa amemaliza kinara baada ya
kufunga mabao sita na kufungana na
Ndombe Mubele wa AS Vita Club ya
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo,
Haythem Jouini wa Esperance de Tunis ya
Tunisia na El Hedi Belameiri wa ES Setif
ya Algeria.
Ni baada ya Ligi ya Mabingwa Afrika
kufikia tamati wikiendi iliyopita na ES
Setif kutangazwa mabingwa wapya
wakibebwa na bao la ugenini kutokana na
matokeo ya sare bao 1-1 mchezo wa
Algeria na sare mabao 2-2 mchezo
uliochezwa Kinshasa.
Ngassa aliyafunga mabao hayo katika
raundi ya kwanza walipocheza na
Komorozine ya Comoro mchezo wa
kwanza walishinda 7-0 na marudiano
walitoka kifua mbele kwa mabao 5-2.
Yanga ilitolewa kwenye mashindano na
Al Ahly ya Misri kwa penalti 3-4. Lakini
Ngassa hawezi kupewa zawadi yoyote
kwavile wamefungana na kiutaratibu
hata mchezaji akishinda tuzo hiyo CAF
huitoa kwa klabu yake.
0 comments:
Post a Comment