INAONEKANA kama uvumilivu
umemshinda, kwani straika wa Yanga,
Jerry Tegete ameomba viongozi wa timu
za Ligi Kuu Bara kuwaruhusu wachezaji
wao kucheza mechi za uswahilini
maarufu kama ndondo ili kulinda vipaji
vyao.
Kauli hiyo ya Tegete imekuja baada ya
klabu nyingi za Ligi Kuu kuwapiga
marufuku wachezaji wao kucheza ndondo
kwa hofu ya kuumia na kupata mzigo wa
kuwatibu wanaporejea katika timu.
Tegete alisema kwa mfano hivi sasa ligi
imesimama na wachezaji wako
mapumzikoni ambako hawawezi
kujibweteka, wanafanya mazoezi katika
timu za mitaani lakini wanapata wakati
mgumu kucheza mechi kwani
hawaruhusiwi na waajiri wao.
Straika huyo anafanya mazoezi binafsi
kutetea nafasi yake Yanga ambayo mmoja
kati ya wachezaji wanaomuweka benchi
ni Genilson Santos ‘Jaja’ wa Brazil.
“Mimi naomba turuhusiwe kucheza mechi
za uswahilini ili kukuza viwango kwani
bila hivyo tutapoteza vipaji vyetu kwani
muda wa wiki nne kukaa bila kucheza si
vizuri.
“Sisi ni binadamu na huku tunapoishi
kuna timu tunazofanya nazo mazoezi sasa
kama umeshiriki mazoezi halafu siku ya
mechi hauendi kucheza hapo hautengenezi
picha nzuri kwa jamii hasa katika
uhusiano, tulipaswa kusisitizwa kucheza
kwa uangalifu tu,” alisema Tegete.
Mara nyingi Tegete huwa anafanya
mazoezi na baadhi ya wachezaji wa Ligi
Kuu na Daraja la Kwanza katika timu ya
Tabata FC kama David Luhende wa
Mtibwa Sugar, Godfrey Taita (Mwadui FC)
na Ivo Mapunda wa Simba.
Kwa mujibu wa habari za ndani, mchezaji
yeyote wa Yanga akithibitika kucheza
ndondo anakatwa Sh400,000 katika
mshahara wake.
0 comments:
Post a Comment