Louis Suarez itabidi awe mpole tu.
Imegundulika kuwa kama akifanya tena
ujinga wake wa kung’ata mtu pale Nou
Camp basi atalambwa dau kubwa la
mshahara wake wa mwaka, hii ni kwa
mujibu wa mkataba wake na Barcelona.
Suarez ambaye ameanza taratibu maisha
yake ya soka Barcelona anachukua dau la
pauni 10 milioni kwa mwaka, lakini
inadaiwa kuwa atakatwa dau la pauni 3
milioni kama akimng’ata mchezaji wa
timu pinzani.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay
tayari amewang’ata wachezaji watatu
katika maisha yake ya soka akichezea
klabu za Ajax, Liverpool na timu yake ya
taifa ya Uruguay.
Novemba 20, 2010 alimng’ata mchezaji
wa PSV, Otman Bakkal katika pambano la
Ligi Kuu ya Uholanzi lililomalizika kwa
suluhu ya bila kufungana. Klabu yake ya
Ajax ilimsimamisha mechi mbili na
kumtoza faini.
Kama vile haitoshi, April mwaka jana
alimng’ata mlinzi wa Chelsea, Branislav
Ivanovic katika pambano la Ligi Kuu ya
England uwanja wa Anfield. FA
ilimfungia mechi 10 za Ligi Kuu ya
englad.
June mwaka huu alimalizia Hat trick
yake ya kung’ata wakati alipomng’ata
mlinzi wa timu ya taifa ya Italia, Giorgio
Chielini katika pambano la kombe la
dunia nchini Brazil. Alifungiwa kucheza
soka kwa miezi minne huku akifungiwa
mechi kumi za timu yake ya taifa ya
Uruguay.
Hata hivyo, baada ya uhamisho huo, staa
huyo alikamilisha uhamisho wa pauni 75
milioni kwenda Nou Camp kutoka Anfield
huku akiingia mkataba wa miaka mitano
ambayo unamfanya alipwe mshahara wa
pauni 200,000 kwa wiki.
Mshahara huo
unamfanya awe mchezaji wa nne kwa
kulipwa zaidi katika klabu ya Barcelona
nyuma ya Lionel Messi, Neymar na
Andres Iniesta, lakini huenda ukashuka
maradufu kama akiendeleza tabia zake za
Ajax na Liverpool.
Mkataba wa Barcelona kwa Suarez ni
mkali na utamuona mchezaji huyo
akipoteza kiasi cha asilimia 15 hadi 30 ya
mshahara kama akirudia kung’ata
wachezaji wa timu pinzani.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa mabosi wa
Barcelona kwa kiasi kikubwa
walishukuru kitendo cha Suarez
kumng’ata Chiellini kwa sababu kwa
kiasi kikubwa kiliharakisha mazungumzo
kati ya timu yao na Anfield.
Kitendo hicho kilishusha thamani ya
Suarez kwa kiasi kikubwa na ni timu
chache ambazo ziliamua kufukuzia saini
yake mara baada ya kung;ata nchini
Brazil.
Kuhakikisha kwamba tukio hilo halitokei
tena, hivi karibuni nyota huyo amekiri
kwamba kwa sasa anapata msaada wa
matibabu ya kisaikolojia kuhakikisha
kwamba hawezi kufanya tena kitendo
hicho katika siku za karibuni.
“Baada ya kufungiwa nilikuwa na wakati
mgumu sana. Napata msaada wa
kisaikolojia na klabu imekuwa ikinisapoti
sana.” alisema mchezaji huyo mwenye
mke na watoto wawili.
Hata hivyo, Suarez amekuwa akipata
sapoti kutoka kwa wanamichezo
mbalimbali duniani licha ya tabia yake
hiyo ya kung’ata. Mmoja kati ya
wanamichezo ambao wamemuunga
mkono ni bondia wa zamani wa uzito wa
Juu Mike Tyson.
“Nadhani zilikuwa hasira za muda tu,
kichwa kilipata moto baada ya
mapambano. Ni suala la kushindwa
kumiliki hasira za muda tu.
Tunakuwa na
hasira za kiushindani na tunakosea
kufikiria vizuri. Wakati mwingine
unachanganyikiwa.” Alisema Tyson.
Tyson mwenyewe aliwahi kukumbwa na
kashfa ya kumng’ata bondia mwenzake
wa uzito wa juu wa Marekani, Evander
Holyfiekld mnamo June 28, 1997.
Mwingine aliyemtetea Suarez alikuwa
mkongwe wa soka duniani, Diego
Maradona ambaye alishutumu zaidi
kifungo cha miezi minne ambacho Suarez
alipewa na Fifa mara baada ya kumng’ata
Chiellini.
“Uamuzi huo ni fedhea. Siwezi kuelewa
kwanini. Suarez amemuua nani hadi
apewe kifungo hiki? Kwanini Fifa
wasimtie pingu na kumpeleka
Guantanamo Bay?” alihoji Maradona
ambaye anasifika kwa misimamo yake ya
kuipinga Fifa mara kwa mara.
“Mchezaji anafanya kazi ngumu mwaka
mzima hili acheze kombe la dunia, Luis
alifunga mabao 29 na wamemuondoa
kombe la dunia kama hivi. Inashangaza
sana.”
0 comments:
Post a Comment