728x90 AdSpace

Tuesday, November 04, 2014

NANI:SIRUDI MANCHESTER UNITED NG'O

WINGA Nani hafikirii kabisa kurudi
Manchester United. Mchezaji huyo
alikwenda Sporting Lisbon kwa mkopo na
kamwe haoni dalili ya kurudi kwenye
kikosi chake.

Ni wazi kuwa kocha mpya wa Man United
Louis van Gaal wala hamfuatilii sana na
Nani ameibuka na kusema hana mpango
na klabu hiyo.

Gazeti moja la Ureno la O Jogo lilimkariri
akitamka: “Ukweli ni kwamba wala sina
mpango wa kurudi kwenye kikosi cha
Man United. Nawapenda watu
wanaonipenda, naamini watu
wanaoamini kuwa nina uwezo wa
kufanya vizuri.

“Nikiwa hapa (Sporting Lisbon) kila
ninapoamka najiona mwenye nguvu zaidi,
kuna viongozi wanaofahamu kuwa nina
uwezo mkubwa na wanataka nionyeshe
kiwango zaidi,” alisema mchezaji huyo
mwenye miaka 27.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: NANI:SIRUDI MANCHESTER UNITED NG'O Rating: 5 Reviewed By: Unknown