Raisi wa chama cha soka cha Ghana Kwesi Nyantakyi amebainisha kuwa sifa na uwezo ndivyo vimefanya Avram Grant 59 aibuke mshindi katika kinyang`anyiro kwa kuwania kitu cha kuinoa timu ya taifa hilo maarufu kama Black Stars.
Grant ambaye ni kocha wa zamani wa vilabu vya Chelsea,Portsmouth na West ham amewabwaga makocha kama Michel Pont naJuan Ignacio Martinez na anatarajiwa kuingia mkataba wa miaka miwili wa kuinoa miamba hiyo ya Afrika Magharibi.
Kwesi Nyantakyi akitangaza matokea amesema...
``Grant ni muhamasishaji.Ni kocha mzuri na mwenye ujuzi mkubwa na pia anajua jinsi ya kukabiliana na changamoto za wachezaji mastaa (Uwajibikaji/Ujivuni) kwani alipokuwa Chelsea aliliweza hilo kitu ambacho kimesumbua makocha wengi waliopita hapa"
0 comments:
Post a Comment