Klabu ya Manchester United imepata pigo jingine baada kiungo wake Muholanzi Delay Blind 24 kupata majeraha jana jumapili wakati akiitumikia timu yake ya taifa dhidi ya Latvia katika mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza michuano ijayo ya Ulaya `Euro 2016'
Blind aliumia misuli kipindi cha kwanza kufuatia kuchezewa vibaya na kiungo wa Latvia Eduards Visnakovs na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo wa Feyenoord Jordy Clasie katika mchezo ulioisha kwa Uholanzi kuitandika Latvia kwa jumla ya mabao 6.
Habari kutoka chama cha soka cha nchi hiyo zinadai kuwa kiungo huyo anayetumia guu la kushoto dimbani atakuwa nje kwa kipindi cha wiki nne mpaka sita hivyo kuikosa safari ya Emirates kuivaa Arsenal.
0 comments:
Post a Comment