Klabu ya Liverpool kupitia kocha wake mkuu Brendan Rogers inapanga kuwapiga bei nyota wake wawili Glen Johnson na Fabio Borin ili kumsajili mlinda mlango wa Stoke City Asmir Begovic mwenye thamani ya £15m hapo mwezi januari mwakani.
Rogers ameonekana kuanza kukatishwa tamaa na kiwango duni kinachoendelea kuonyeshwa na mlinda mlango wake namba moja Simon Mignolet hasa baada ya hivi karibuni kupwaya katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya klabu ya Ludogorets ya Bulgaria.
Liverpool inamuona Begovic 27 raia wa Bosnia aliyeichezea Stoke City zaidi ya michezo 150 ya ligi kuu kuwa ndiye mtu sahihi katika kutoa ushindani kwa Mignolet aliyetua klabuni hapo miezi 18 iliyopita akitokea klabu ya Sunderland.
Habari zaidi zinasema iwapo Liverpool itashindwa kumnasa Begovic itahamia kwa Peter Cech mlinda mlango wa klabu ya Chelsea ama Neto wa Fiorentina ya Italia.
0 comments:
Post a Comment