Mlinda mlango wa zamani wa klabu ya Arsenal David Seaman ameitaka klabu hiyo kuachana na mpango wa kumsajili mlinda mlango wa klabu ya Chelsea Peter Cech na badala yake iendelee kumwamini Wojciech Szczesny kwa kuwa hafanyi makosa.
Seaman ambaye aliichezea Arsenal kwa mafanikio makubwa anaamini kuwa Szczesny 24 ni mmoja kati ya walinda mlango bora zaidi kwa sasa licha ya kuwa mpaka sasa amesharuhusu kufungwa magoli mengi.
Akifanye mazungumzo na Talkspot Seaman amesema
`` Wojciech Szczesny ni mlinda mlango mzuri sana ikumbukwe msimu uliopita yeye na Peter Cech kwa pamoja waliibuka kidedea baada ya kucheza michezo 17 ya ligi kuu bila ya kufungwa".
Kutaka kumsajili mlinda mlango mwingine kwa kigezo kuwa Wojciech Szczesny ameshuka kiwango ni kumkosea heshima.Kweli Arsenal mpaka sasa wamefungwa magoli mengi lakini ukitazama utagundua kuwa makosa siyo yake bali ni ya safu ya ulinzi hivyo hapaswi kubadilishwa ama kuwekwa benchi"
0 comments:
Post a Comment