728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, November 17, 2014

    RAISI BARCELONA ATUPWA JELA KWA RUSHWA

    Raisi wa zamani wa klabu ya Fc Barcelona Jose Nunez ameanza kutumikia kifungo cha miaka miwili na miezi miwili jela kwa kosa la kutoa rushwa.

    Nunez 83 ambaye aliiongoza Barcelona 1978-2000 alikutwa na kosa hilo mwaka 2011 baada ya kujaribu  kutoa rushwa kwa afisa mmoja wa kodi ili kukwepa ukaguzi katika kampuni yake ya ujenzi.

    Mapema jana jumapili televisheni ya Antena 3 ilimuonyesha Nunez akiwasili katika jela ya Quatre Camins ili kuanza kifungo hicho baada ya hapo novemba 6 kupewa siku 10  na mahakama za kuanza kifungo hicho.

    Nunez anaanza kifungo hicho baada ya rufaa yake kutupwa lakini amefaulu kupunguziwa adhabu tuko miaka sita mpaka miwili.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RAISI BARCELONA ATUPWA JELA KWA RUSHWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top