Kiungo wa timu ya taifa ya Wales Aaron Ramsey ameibuka na kudai kuwa taratibu ameanza kurejea kwenye kiwango chake cha msimu uliopita.
Ramsey ambaye jana jumapili aliiongoza timu yake ya taifa kuibana na hatimaye kwenda sare na timu ya taifa ya Ubelgiji katika mchezo mkali wa kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya Euro 2016 katika dimba la King Baudoui,Wales amesema
``Naufahamu uwezo wangu,najua kile ninachotakiwa kufanya kama mchezaji"
``Kwakweli bado sijawa fiti asilimia mia moja,nimekuwa na majeraha ya mara kwa mara lakini nikijitazama kwa sasa naona kabisa kiwango changu kinaanza kuimarika tena"
Katika siku za hivi karibuni Ramsey amejikuta katika wakati mgumu kufuatiwa kukosolewa mara kwa mara hasa na kocha Arsenal kutokana na tabia ya kupenda kufunga zaidi kuliko kuunganisha timu.
0 comments:
Post a Comment