Kocha mkuu wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers amelia na mwamuzi Antony Taylor kufuatia mwamuzi huyo kushindwa kutoa penati baada ya mlinzi wa Chelsea Garry Cahill kuzuia kwa mkono shuti la Steven Gerrard lililokuwa likielekea golini na timu yake kuambulia kipigo cha magoli 2-1 toka kwa Chelsea mchana wa leo Anfield.
Rodgers akifanya mahojiano na BBC amesema
``Taylor ametunyima penati ya wazi kabisa.Nimehuzunika sana,wachezaji wamejitolea kwa moyo wote kupata ushindi lakini mwamuzi yametunyima kupata japo sare" alimaliza kocha huyo mtaratibu.
0 comments:
Post a Comment