Timu ya mpira wa miguu ya Corinthians nchini
Brazil inatarajiwa kufungua eneo la makaburi
kwa ajili ya mashabiki wake ambao wanataka
kuzikwa karibu na wachezaji wao maarufu.
Mashabiki wataweza kuchagua vitalu hadi
kufikia 70,000 katika eneo la "Corinthians
Forever" yaani "Wakarintho Milele" karibu na
jiji la Sao Paulo.
Eneo hilo pia litatumika kama mahali pa
pumziko la milele kwa baadhi ya wachezaji
maarufu wa timu hiyo.
Timu ya Corinthians ni ya pili kwa kuwa na
wingi wa mashabiki wanaofikia milioni 25
nchini kote Brazil.
Eneo hilo la makaburi litakuwa na vyumba
vya shughuli, bustani, mgahawa, ziwa na
msitu wa hifadhi, amesema Ricardo Polito,
afisa mtendaji mkuu wa kampuni
inayosimamia mradi huo.
Shabiki wa timu ya Corithians ya Brazil
akiomba dua kwa ajili ya timu yake.
Mashabiki wa timu ya Corinthian,
wanaojiita"watiifu" - lakini wanajulikana na
mashabiki wa timu pinzani kuwa"genge la
vichaa"- kwa sasa watapata fursa ya
kuendeleza ushabiki wao milele.
Waandishi wa habari wanasema mashabiki wa
Corinthians wataungana na kundi dogo la
klabu nyingine za mpira wa miguu ambazo
zinatoa eneo la kuzika mashabiki, ikiwemo
Boca Juniors kutoka Argentina.
Vitalu vya makaburi vitagharimu kati ya dola
za Kimarekani $1,870 na $3,240)
kutegemeana na eneo la makaburi
lililochaguliwa na ukaribu wake na watu
maarufu wa klabu hiyo ambao nao watazikwa
hapo.
Wanaounga mkono hatua hiyo wanasema ni
jambo jema kuwapa nafasi hiyo mashabiki
wanaojulikana kwa moyo wa mapenzi kwa
timu hiyo.
Mwezi uliopita, timu ya Corithians ilipewa
onyo na mamlaka kwa kuitaka kuwazuia
mashabiki wake kutotoa lugha ya matusi kwa
timu pinzani, hususan wapinzani wa jadi timu
ya Sao Paulo, ambayo mlinda mlango wake
amekuwa akitukanwa.
0 comments:
Post a Comment