Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya England na klabu ya Tottenham Hotspurs Paul Gascoigne Gazza 47 ameibuka na kusema kuwa klabu ya Arsenal na kocha wake Arsene Wenger ndiyo siri ya yeye kuendelea kupumua kwa raha.
Gazza akifanya mahojiano na gazeti la The Sun hivi karibuni baada ya kutoka katika kituo cha matibabu ya watu wenye matatizo ya ulevi/ugonjwa wa akili amesema
``Nilimpigia simu daktari wa klabu ya Arsenal Gary Lewin na kumwambia sijisikii vizuri kiafya,akanishauri niende hospitali.Taarifa hizo zilipomfikia Wenger akanipatia £28,000 huku Arsenal ikiongeza £22,000 na jumla kuwa £50,000 ambaye imenisaidia kutibu matatizo niliyokuwa nayo.Kuna wakati huwa najiuliza kwanini Arsenal waliamua kutoa pesa zile wakati sijawahi kuwa mchezaji wao wakati huo huo nikichezea timu pinzani ya Tottenham?Kwakweli nimeshangazwa sana.Nashukuru naendelea vizuri kwa sasa.
Pia Gazza alifichua kwamba klabu yake ya zamani jinsi ilivyotia ugumu kwa yeye kuingia katika dimba la White Hart Lane kutazama mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Real Madrid
Anasema `` Nilifika uwanjani kutazama mchezo huo lakini nilizuiwa na kuambiwa lazima nilipie tiketi ndipo niruhusiwe kuingia.Kulikuwa na tiketi mbili za £60
0 comments:
Post a Comment