Metz,Ufaransa.
UFARANSA imemaliza kwa kishindo maandalizi yake ya kujiandaa na michuano ya EURO baada ya Jumamosi usiku kuichapa Scotland kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa katika dimba la Stade Saint-Symphorien,Metz-Ufaransa.
Ufaransa ilianza kujihakikishia ushindi dakika ya 8 tu ya mchezo baada ya mshambuliaji wake Olivier Giroud kufunga kwa kisigino akimalizia krosi ya mlinzi wa kulia Bacary Sagna.
Dakika ya 27 Ufaransa ilipata bao la pili mfungaji akiwa ni Olivier Giround kwa mara nyingine.Giroud alifunga bao hilo baada ya kumalizia mpira uliotemwa na kipa wa Scotland David
Marshall uliotokana na mkwaju mkali wa Dimitri Payet.
Mabao hayo yamemfanya Giroud awe ameifungia Ufaransa mabao 17 katika michezo 49.Mabao sasa akiyafunga katika michezo saba ya hivi karibuni.
Dakika ya 39 Ufaransa ilipata bao la tatu baada ya beki wake Laurent Koscielny kufunga kwa kichwa akiunganisha kona ya kiungo Dimitri Payet.Bao hilo ni la kwanza kwa Koscielny kuifungia Ufaransa.
Ufaransa itacheza mchezo wake wa kwanza wa fungua dimba ya michuano ya Euro wa kundi A Ijumaa katika dimba la Stade de France kwa kuvaana na Romania.Timu nyingine zinazounda kundi A ni Albania na Uswisi.
VIKOSI
Ufaransa: Lloris; Sagna, Rami,Koscielny, Evra (Digne 83); Pogba,Kante (Sissoko 88), Matuidi (Cabaye 69); Payet (Martial 46), Coman (Griezmann 46), Giroud (Gignac 63)
Scotland: Marshall; Martin, Greer,Hanley, Robertson (Mulgrew 46);McArthur (McKay 84), Fletcher;Snodgrass (Kingsley 66), Maloney (Anya 46), Ritchie; Fletcher (Naismith 58)
0 comments:
Post a Comment