728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 05, 2016

    BRAZIL YAANZA KICHOVU COPA AMERICA CENTENARIO YATOKA SARE NA ECUADOR

    Los Angels,Marekani.

    Timu ya taifa ya Brazil imeianza kinyonge michuano ya Copa America Centenario baada ya kutoka sare ya bila kufungana na timu ya taifa ya Ecuador katika mchezo mkali wa kundi B uliochezwa alfajiri ya leo katika uwanja wa Ross Bowly huko Los Angels,Marekani.

    Brazil licha ya kumiliki mpira kwa asilimia 53 ilijikuta ikisaka mabao bila kufanikiwa kutokana na Ecuador kusimama imara muda wote wa mchezo 

    Ecuador nusura itoke kifua mbele katika mchezo huo kama siyo mwamuzi kukataa bao la mshambuliaji Enner Valencia kwa madai kuwa mpira ulikuwa umetoka kabla ya kumfikia mfungaji.

    Katika michezo ya mapema kutoka kundi A:Costa Rica na Paraguay zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bila kufungana huku katika mchezo mwingine wa Kundi B,Haiti imeangukia pua baada ya kuchapwa bao 1-0 na Peru.Bao la Peru limefungwa dakika ya 61 na Paolo Guererro.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BRAZIL YAANZA KICHOVU COPA AMERICA CENTENARIO YATOKA SARE NA ECUADOR Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top