Petrovski enzi za uhai wake
Malacca,Malaysia.
Mlinda mlango chipukizi raia wa Australia Stefan Petrovski amefariki dunia jana Jumapili baada ya kupigwa na radi huko Melacca,Malaysia.
Petrovski,18 na beki Muhd Afiq Azuan,21 walipigwa na radi Aprili 5 wakati wakifanya mazoezi na wachezaji wenzao wa klabu ya Melacca United.
Msemaji wa hospital ya Putra Specialist Hospital alikokuwa amelazwa Petrovski amesema mlinda mlango huyo amefariki Jumapili saa 4.40pm baada ya kudumu hospitalini hapo akiwa hajitambui kwa kipindi cha karibia mwezi mmoja.
Vipimo vilionyesha Petrovski alipata tatizo linaloitwa Cerebral Hypoxia Ischemia ambalo husababishwa na ubongo kukosa okisijeni (oxygen) ya kutosha.Pia alipata tatizo liitwalo Cerebral Edema,ubongo kuvimba.
Wakati huohuo msemaji huyo ameongeza kuwa Muhd Afiq Azuan,21ambaye nae alipigwa na radi siku hiyo hali yake inaendelea vizuri.
Petrovski alijiunga na Melacca United hivi karibuni na kufanikiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu akitokea klabu ya Sydney Olympic ya nyumbani kwao Australia.
Petrovski akiwa hospitalini Putra
0 comments:
Post a Comment