Mwendwa akiteta jambo na Amrani
Nairobi,Kenya.
Kenya itawania uenyeji wa michuano ya soka ya mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON ya mwaka 2025 hii ni kwa mujibu wa Rais wa chama cha soka cha nchi hiyo (FKF) Nick Mwendwa.
Mwendwa ameyasema hayo wakati akihitimisha ziara ya siku tatu iliyofanywa na Katibu mkuu wa CAF Hicham El Amrani na makamu wa Rais wa CAF Almay Kabele Kamara maalumu kwa ajili ya ukaguzi wa viwanja na mambo mengine tayari kwa uenyeji wa michuano ya tano ya CHAN ya mwaka 2018.
Mwendwa amesema "Tunatarajia kufanya makubwa ikiwemo kuboresha miundo mbinu ya viwanja vyetu.Ikiwa tutafanikiwa kuandaa vyema michuano ya CHAN naamini tutakuwa na ubavu wa kuingia katika kinyang'anyiro cha kuwania uenyeji wa AFCON ya mwaka 2025 na kushinda.
Tumelenga 2025 kwa kuwa michuano yote ya hapa katikati tayari imeshapata waandaaji."
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Kenya kutaka kuwa mwenyeji wa michuano ya AFCON.Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1996 ilipozidiwa ujanja na Afrika Kusini baada ya serikali ya nchi hiyo kushindwa kutoa sapoti ya kutosha.
Mbali ya Kenya nchi nyingine ya Afrika Mashariki iliyoonyesha nia ya kuwania uenyeji wa michuano hiyo ni Rwanda,Tanzania vipiiiiiiii???
0 comments:
Post a Comment