728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 02, 2016

    KIPIGO CHA INTER TOKA KWA LAZIO CHAZINUFAISHA ROMA,NAPOLI.

    Roma,Italia.

    Vilabu vya Roma na Napoli vimeungana Juventus kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu ujao wa 2016-17 baada ya Jumapili usiku Inter Milan kukubali kichapo cha mabao 2-0 toka kwa Lazio  katika mchezo wa ligi ya Seria A uliopigwa huko Stadio Olimpico.

    Mabao yaliyofuta ndoto za Inter Milan kurejea Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuikosa kwa kipindi kirefu yametiwa kimiani na mkongwe Miroslav Klose dakika ya dakika ya 8 ya kipindi cha kwanza huku lile la pili likitiwa kimiani kwa mkwaju wa penati na nahodha Antonio Candreva baada ya Keita kuangusha kwenye eneo la hatari na mlinzi Jeison Murillo.

    Kwa matokeo hayo tumaini pekee la Inter Milan limebaki katika michuano midogo ya Ulaya maarufu kama Europa Ligi huku ikiziacha Roma na Napoli zikigombea nafasi ya kufunzu Ligi ya Mabingwa moja kwa moja na ile ya kuingia kupitia mtoano.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KIPIGO CHA INTER TOKA KWA LAZIO CHAZINUFAISHA ROMA,NAPOLI. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top