728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 02, 2016

    FARID MUSA AONGEZEWA MUDA WA MAJARIBIO HISPANIA


    Tenerife,Hispania.

    WINGA mahiri wa timu ya Azam FC, Farid Musa,ameongezewa muda wa wiki moja kuendelea kufanya majaribio kwenye klabu ya Deportivo Tenerife ya Hispania.

    Hali hiyo imetokana na winga huyo kulivutia benchi la ufundi la klabu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini humo maarufu kama La Liga Segunda.

    Farid ambaye alitarajia kufanya majaribio katika timu hiyo kwa wiki tatu, hivyo atalazimika kuongeza wiki moja na jumla kuwa nne zitakazomfanya kurejea nchini Mei 26 mwaka huu.

    Kwa mujibu wa tovuti ya Azam, Mjumbe wa Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo, Yusuf Bakhresa ambaye yupo Tenerife, alisema Farid alishafanyiwa vipimo vya afya baada ya kuwavutia viongozi wa benchi la ufundi la Tenerife linaloongozwa na Kocha Mkuu, Jose Luis Mart.

    “Kiwango cha Farid kimeivutia timu ya Tenerife na iko tayari kumsajili kwa mkopo wa miaka miwili endapo atafuzu vipimo vya afya,” alisema Bakhresa.

    Pia aliongezea kuwa uwepo wa Farid nchini Hispania unamfanya akose michezo iliyobaki kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: FARID MUSA AONGEZEWA MUDA WA MAJARIBIO HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top