728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 02, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA 10 ZA USAJILI TOKA ULAYA JUMATATU YA LEO MEI 2,2016.

    Samuel Umtiti

    Yarmolenko: Rais wa Dynamo Kiev ya Ukraine Ihor Surkis amesema hawezi kuacha staa wake  Andriy Yarmolenko,26 ajiunge na vilabu vidogo kama Everton ama Stoke City.Atajiunga na vilabu vinavyoshiriki michuano mikubwa pekee,alisema Surkis.(UNIAN)Liverpool ni moja kati ya vilabu vinavyopigiwa chapuo kumnasa mkali huyo wa kupiga vyenga.

    Umtiti:Mlinzi wa kati wa Lyon Mcameroun Samuel Umtiti,22 yuko tayari kukataa ofa ya kutua Tottenham ili kusubiri ofa toka vilabu vya Hispania ambako ndiko anaamini soka lake linapofaa .Msimu huu Umtiti ameichezea Lyon michezo 35 na kuifungia bao moja.(Daily Mirror)

    Tierney:Arsenal imeripotiwa kutenga kitita cha £5m kwa ajili ya kutaka kumsajili mlinzi wa kushoto wa Celtic Kieran Tierney,18. Mbali ya Arsenal Tierney pia ametajwa kuvivutia vilabu vya Liverpool na Manchester City.(Daily Star)

    Mikel:Kiungo John Obi Mikel amekataa ofa nono ya mshahara wa £110,000 kwa wiki toka katika klabu ya Fenerbahce ya Uturuki ili asalie kunako klabu yake ya sasa ya Chelsea licha ya mkataba wake kubakisha miezi 12 kuisha.(The Sun)

    Ronaldo:Staa wa Real Madrid Mreno Cristiano Ronaldo anataka kuona kocha wa sasa wa klabu hiyo Mfaransa Zinedine Zidane anabakia Santiago Bernabeu kwa muda mrefu zaidi.(Mundo)

    Pellegrini:Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini ameripotiwa kukataa ofa ya kufundisha soka katika mataifa ya China, Qatar na Russia ili abaki England anakohusishwa kutakiwa na vilabu vya Arsenal, Everton na Watford.(Daily
    Mail)

    Caceres:Roma imeonyesha nia ya kutaka kumsajili kwa uhamisho huru mlinzi wa kulia wa Juventus Mruguayi Martin Caceres. Caceres,29 ataondoka Juventus mwishoni mwa msimu huu akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kufikia ukingoni.(Gazzetta dello Sport)

    Griezmann: Manchester United imeripotiwa kuandaa kitita cha £135m ili kuwasajili kwa mpigo washambuliaji Antoine Griezmann na Pierre-Emerick Aubameyang.(The Sun)

    Musa:Leicester City imefufua upya mbio za kumuwania mshambuliaji wa CSKA Moscow Mnigeria Ahmed Musa mwenye thamani ya £20m tayari kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hapo msimu ujao.(Daily Mail)

    Cazorla:Baada ya kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao Villarreal ina matumaini ya kumshawishi staa wake wa Santi Cazorla ahame Arsenal na kurejea El Madrigal kwa mara ya tatu.(Daily Star)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA 10 ZA USAJILI TOKA ULAYA JUMATATU YA LEO MEI 2,2016. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top