728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 02, 2016

    JAMIE VARDY ATWAA TUZO NYINGINE TENA ENGLAND

    Leicester, England.

    Mshambuliaji wa mahiri wa Leicester City Muingereza Jamie Vardy muda mchache uliopita ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa chama cha waandishi wa habari za michezo FWA (Football Writers' Association).

    Vardy,28 ambaye mapema wiki iliyopita alipewa tuzo maalumu baada ya kuweka rekodi ya kufunga mabao katika michezo 11 ya michezo ya Ligi Kuu England ametwaa tuzo ya FWA baada ya kuwashinda nyota wenzie wa Leicester City N'Golo Kante na Ryad Mahrez.

    Nyota wengine walioingia katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hiyo na kutoka kapa ni Danny Drinkwater, Danny Simpson, Wes Morgan,Kasper Schmeichel,Mesut Ozil na Harry Kane.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: JAMIE VARDY ATWAA TUZO NYINGINE TENA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top