Kijana Mtanzania Emily Mugeta amesaini mkataba wa mwaka
mmoja na klabu ya Neckarsulm ya daraja la chini ya VERBANSLIGA ya nchini Ujerumani.
Beki huyo kinda wa Simba SC amesaini mkataba
huo baada ya kufuzu majaribio yaliyofanyika majuma mawili yaliyopita.
“Nimesaini mwaka mmoja, nilifanya
majaribio na kufuzu na sasa naangalia namna nitakavyopambana,” alisema beki
huyo wa kushoto kutoka Ujerumani alipozungumza na Saleh Jembe
Mgeta ni mmoja wa vijana waliokuwa
katika kikosi cha akina Said Ndemla, Ramadhani Singano ‘Messi’ na wengine.
0 comments:
Post a Comment