Baba yake mshambuliaji wa Yanga, Happygod Msuva, mkewe Suzan James
na binti yao Mary ambaye ni dada wa Msuva wakipokea zawadi ya mchezaji bora wa
Tanzania Bara aliyoshinda Msuva.
Wazazi na dada yake Msuva walikabidhiwa tuzo hiyo na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia ambaye aliwahi kuwa Katibu Mwenezi wa Simba.
Msuva ameshinda tuzo hiyo kwa kuwapiku Mrisho Ngassa na beki wa
Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
0 comments:
Post a Comment