Chelsea imeripotiwa kufanikiwa kushinda mbio za kumsajili kipa mkongwe Marco Amelia toka Italia aliyekuwa pia akipigiwa hesabu na Arsenal.
Amelia anatarajiwa kusaini kuichezea Chelsea leo ijumaa kwa mkataba wa msimu mmoja baada ya kufaulu majaribio aliyofanya wiki iliyopita.Chelsea iliamua kumgeukia Amelia aliyekuwa huru baada ya kipa wake namba moja Thibaut Courtois kufanyiwa upasuaji kufuatia kupata jeraha la goti mwanzoni mwa msimu huu.
Amelia,33 ameshacheza michezo 317 akiwa na vilabu vya Livorno, Palermo, Genoa na AC Milan huku mwaka 2006 akiwa katika kikosi cha Italia kilichotwaa kombe la dunia nchini Ujerumani wakati huo kikiwa chini ya kocha Marcello Lippi.
0 comments:
Post a Comment