Ayoze Perez
Na.sokaextra.blogspot.com
Kessy:Azam FC imeripotiwa kuipiku Yanga katika mbio za kutaka kumsajili mlinzi wa kulia wa Simba Hassani Kessy baada ya kudaiwa kukaribia kumalizana nae masuala yote ya kimsingi ikiwemo dau la usajili.(Saleh Ally)
Mbonde:Mlinzi wa Mtibwa Sugar Salum Mbonde amesema atajiunga na klabu yoyote ile ya ligi kuu bara ikiwa tu itamuwekea mezani kitita cha Tshs 20m.(Saleh Ally)
Mourinho:Manchester United imemwambia Jose Mourinho atapewa kibarua cha kuinoa klabu hiyo pindi mkataba wa kocha wake wa sasa Louis van Gaal utakapokuwa umefikia tamati mwaka 2017.(The Sun)
Zuttah:Mlinzi aliyecheza Yanga kwa muda mfupi mwaka jana, Mghana Joseph ‘Teteh’ Zuttah yuko mbioni kusajiliwa na ZweKapin United FC yenye maskani yake Burmese, Hpa-An,Myanmar.(Binzubery)
Higuain:Mshambuliaji wa Napoli Muargentina Gonzalo Higuain amesema yuko tayari kujiunga na Chelsea kwa ada ya £42m ikiwa tu klabu hiyo ya London itamuuza mshambuliaji wake Diego Costa mwishoni mwa msimu huu.(Sun )
Drinkwater:Vilabu vya Liverpool na Chelsea vimeripotiwa kuanza kutiana pembe katika mbio za kumuwania kiungo wa Leicester City Muingereza Danny Drinkwater,26 ambaye mkataba wake utafikia mwisho mwaka 2018.(La Gazzetta dello Sport)
Benteke:Kocha wa Leceister City Claudio Ranieri ameripotiwa kutaka kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao kwa kuwasajili Christian Benteke (Liverpool),Kostas Manolas (AS Roma) na winga wa Borussia Monchengladbach Thorgan Hazard.(Gazzetta dello Sport)
Matic:Juventus iko katika hatua nzuri ya kumsajili kiungo Nemanja Mataic kwa ada ya £20m baada ya Chelsea kuonyesha nia ya kumuuza nyota huyo wa zamani wa Benfica.(Daily Express)
Ayoze: Barcelona imedaiwa kuanza kumfukuzia mshambuliaji kinda wa Newcastle Muhispania Ayoze Perez,22 ili kuwa msaada pindi nyota wake Lionel Messi, Neymar na Luis Suarez wanapoonekana kuchemsha.(Daily Mirror)
Griezmann:Atletico Madrid imeripotiwa kupandisha bei ya mshambuliaje wake Mfaransa Antoine Griezmann.Klabu yoyote itakayomtaka Griezmann itapaswa kutoa kitita cha £79m.(The Sport Review)
Icard:Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ameripotiwa kuwa atafunga safari mpaka Italia kwenda kumtaza mshambuliaji wa Inter Milan Muargentina Mauro Icardi,24 kwenye michezo iliyobaki ya Seria A kabla ya kuamua kumsajili pindi dirisha la usajili barani Ulaya litakapofunguliwa.(Metro)
El Ghazi:Liverpool inaandaa dau kwa ajili ya kumsajili winga wa Ajax Anwar El Ghazi ( Express)
0 comments:
Post a Comment