Madrid,Hispania.
Ushindi bao 1-0 iliyoupata Real Madrid Jumatano usiku dhidi ya Manchester City katika mchezo wa pili wa nusu fainali umeifanya klabu hiyo ya Santiago Bernabeu iifikie rekodi ya Arsenal ya kucheza michezo kumi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya bila ya kuruhusu bao katika goli lake.
Arsenal ilikuwa klabu ya kwanza kuweka rekodi hiyo msimu wa 2005-06 pale ilipocheza michezo kumi ya Ligi ya Mabingwa bila ya kuruhusu bao kabla ya kufungwa mabao 2-1 na FC Barcelona katika mchezo wa fainali.
Real Madrid itavaana na mahasimu wao wakubwa Atletico Madrid katika mchezo wa fainali utakaochezwa Mei 28 huko San Siro,Italia.
Hii itakuwa ni mara ya nne kwa mchezo wa fainali kuchezwa katika uwanja huo ulioanza kutumika 19 Septemba 1926.Fainali zilizopita ni zile za 1965,
1970 na 2001.
0 comments:
Post a Comment