728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 04, 2016

    MESSI AMPONZA MTOTO WA KIAFGHANISTANI SASA AANZA KUWINDWA KAMA KUKU AUAWE

    Quetta,Pakistani.

    Unamkumbuka yule mtoto wa miaka mitano wa Kiafghanistani Murtaza Ahmadi aliyepata umaarufu mkubwa duniani baada ya picha zake kusambaa mitandaoni zikimuonyesha akiwa amevaa mfuko wa rambo (plastiki) uliotengenezwa na kufanana na Jezi za timu ya taifa ya Argentina huku  ukiwa na jina la Lionel Messi??

    Walimwengu hawana maana!!

    Sasa taarifa ziko hivi Murtaza Ahmadi ametoroka huko nyumbani kwao katika jimbo la Ghazni,Afghanistani akiambatana na wazazi wake na kwenda kuishi Quetta,Pakistani baada ya kuanza kupokea vitisho vya kuuwawa.

    Baba mzazi wa Murtaza aitwaye, Arif, ameliambia The Daily Telegraph kuwa Tangu Murtaza awe maarufu duniani yeye na familia yake wamekuwa wakipokea vitisho vingi toka kwa makundi mbalimbali ya kigaidi, waharifu na wababe wa kivita wa Afghanistani.

    "Nina hofu Murtaza anaweza akatekwa na hata kuuwawa.Tumeamua kukimbilia Pakistani kwa ajili ya usalama wake na wetu kwani tumekuwa tukipokea vitisho vya kila namna" Alimaliza Arif.

    Miezi minne iliyopita jina la Murtaza Ahmadi liligonga vichwa vya habari vya mitandao mbalimbali dunia na hata kumfikia Lionel Messi mwenyewe.

    Katika kuonyesha kuwa na yeye ameguswa na upendo wa Murtaza juu yake Messi amtumia mtoto huyo jezi yake  halisi huku akiweka ahadi ya kukutana nae siku moja.


    Mtoto Murtaza akiwa na Jezi aliyopewa na Messi 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MESSI AMPONZA MTOTO WA KIAFGHANISTANI SASA AANZA KUWINDWA KAMA KUKU AUAWE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top