Lyon,Ufaransa.
HATIMAYE Memphis Depay amefunga bao lake la kwanza akiwa na klabu yake mpya ya Lyon katika ushindi wa mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Nancy jana Jumatano usiku huko Parc Olympique Lyonnais.
Depay ambaye alianzia benchi katika mchezo huo kisha akaingia uwanjani dakika tano kabla ya mapumziko kuchukua nafasi ya Mathieu Valbuena aliyepata majeraha hakupoteza muda kwani katika dakika ya 54 aliizawadia Lyon mkwaju wa penati uliofungwa na Alexandre Lacazette na kufanya matokeo yawe 3-0.
Kabla ya hapo Lyon tayari ilikuwa mbele kwa mabao 2-0 ya Mathieu Valbuena pamoja na Nabil Fekir.
Depay alihitimisha karamu ya mabao baada ya kufunga bao la nne kwa mkwaju mkali wa karibu uliomshinda kipa wa Nancy,Sergei Chernik na kujaa wavuni.Pasi ikitoka kwa Maxime Gonalons.
Katika mchezo mwingine Dimitri Payet nae amefunga bao lake la kwanza kwa mkwaju wa faulo akiwa na Marseille katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Guingamp.Bao jingine la Marseille limefungwa na Bafetimbi Gomis.
0 comments:
Post a Comment