Turin,Italia
MUARGENTINA Paulo Dybala (Pichani Juu) amefunga mabao mawili na kupika moja katika ushindi wa Juventus wa mabao 4-1 dhidi ya timu yake ya zamani ya Palermo katika mchezo pekee wa Seria A uliochezwa Ijumaa usiku huko Juventus Arena.
Mabao mengine ya Juventus yamefungwa na kiungo Claudio Marchisio aliyekuwa anafunga bao lake la kwanza tangu mwaka 2015 pamoja na Gonzalo Higuain ambaye sasa amefikisha mabao 19 msimu huu.Bao la Palermo limefungwa na Ivaylo Chochev.
Ushindi huo umeifanya Juventus sasa ifikishe pointi 63 kilele baada ya kushuka dimbani mara 25,pointi kumi mbele ya AS Roma wanaoshika nafasi ya pili.
0 comments:
Post a Comment