728x90 AdSpace

Sunday, February 26, 2017

Zlatan Ibrahimovic aipa Man United kombe la Ligi





 London, England.

Zlatan Ibrahimovic ameifungia Manchester United mabao mawili na kuiwezesha kutwaa kombe la ligi (EFL) baada ya kuichapa Southampton kwa mabao 3-2 katika mchezo wa fainali uliisha hivi punde kwenye dimba la Wembley jijini London.

Ibrahimovic,35,alianza kuifungia Manchester United bao la kuongoza kwa mkwaju mkali wa adhabu uliomwacha kipa wa Southampton Fraiser Froster akichupa bila mafanikio.

Tokeo la picha la man utd 3-2 southampton

Ibrahimovic aliipatia bao la ushindi Manchester United katika dakika ya 87 ya mchezo kwa kichwa akiunganisha krosi safi ya kiungo,Ander Herrera.Bao jingine la Manchester United limefungwa na kinda,Jesse Lingard.

Mabao yote ya Southampton yamefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Italia,Manolo Gaddiadini 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Zlatan Ibrahimovic aipa Man United kombe la Ligi Rating: 5 Reviewed By: Unknown