London,England.
Wenger:Kocha wa Arsenal,Arsene Wenger amesema bado ana miaka minne ya kuendelea kufundisha soka la ushindani na kusisitiza kuwa angependa miaka hiyo yote aimalizie akiwa klabuni hapo.(Daily Mirror)
Keane:Rio Ferdinand ameitaka Manchester United kumsajili tena mlinzi wake wa zamani,Michael Keane ambaye kwa sasa yuko Burnley na kusisitiza kuwa usajili wa Paul Pogba mwaka 2016 unadhihirisha kwamba Manchester United haiogopi kujisahihisha pindi inapotambua imefanya makosa.(The Guardian)
Rodriguez:Inter Milan imeshinda vita ya kumwania mlinzi wa kushoto wa Wolfsburg, Ricardo Rodriguez ambaye pia alikuwa akiwaniwa na vilabu vya Arsenal na Chelsea.Inter Milan imekubali kutoa €22m.(Gazetta dello Sport)
Mendy:Manchester City inafikiria kumsajili mlinzi wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy ili kuchukua nafasi ya mkongwe,Gael Clichy ambaye hatapewa mkataba mpya pindi ule wa sasa utakapoisha mwezi Juni.(The Sun)
Klopp:Jurgen Klopp amekiri kuwa tayari Liverpool imeshaanza mazungumzo na wachezaji kadhaa tayari kwaajili ya kuwasajili katika dirisha lijalo huku kiungo wa Bayer Leverkusen,Julian
Brandt akiwa chagua namba moja.(Daily Mirror)
Solanke:Liverpool imejitoa kwenye mbio za kumwania kinda wa Chelsea,Dominic Solanke na kuziacha Arsenal na Sunderland zikiendelea kutoana jasho kumwania kinda huyo aliyegomea mkataba mpya Stamford Blidge.
Belotti:Bayern Munich imeungana na Manchester United,Chelsea na Arsenal katika mbio za kumwania straika mahiri wa Torino ya Italia,Andrea Belotti.(The Sun)
Chamakh:Straika wa zamani wa Arsenal na Crystal Palace,Marouane Chamakh,yuko mbioni kujiunga na Vicenza Calcio inayoshiriki ligi daraja la pili Italia.(Di Marzio)
Dahoud:Chelsea inakabiriwa na upinzani mkali kutoka kwa Borussia Dortmund,Paris Saint-Germain na Juventus katika mbio za kuinasa saini ya kiungo wa Borussia Monchengladbach,Mahmoud Dahoud (The Guardian)
Adrian:Mlinda mlango wa West Ham,Adrian,ameripotiwa kuwa atakataa kusaini mkataba mpya na angependelea kurejea nyumbani kwao Hispania katika dirisha lijalo la usajili.(Claret & Hugh)
Murillo:Inter Milan inataka kumpa mkataba mpya mlinzi wake mahiri kutoka Colombia,Jeison Murillo,ili kuvipunguza kasi vilabu vya England ambayo vimekuwa vikimtolea macho kila kukicha.(Daily Express).
Ballo-Toure:Vilabu vya West Ham,Tottenham,Liverpool, Everton,Aston Villa na Brighton katika nyakati vimeripotiwa kumnyatia mlinzi wa Paris St-Germain,Fode Ballo-Toure,20,anayemaliza mkataba wake mwezi Juni.(Madein Foot)
Wayne:Manchester United bado ina nafasi ya kumuuza Wayne Rooney kwenda China kabla ya dirisha la usajili halijafungwa mwishoni mwa mwezi huu.(A Bola)
0 comments:
Post a Comment