Manchester, England.
MANCHESTER CITY imeripotiwa kutenga kitita cha £140m kwa ajili ya kuwanasa nyota wanne wa AS Monaco katika dirisha lijalo la usajili barani Ulaya.
Nyota wanaodaiwa kutengewa kitita hicho kikubwa cha fedha ni pamoja na Kinda Kylian Mbappe,18, ambaye thamani yake inadaiwa kuwa ni £50m.
Jina la Mbappe ambaye kiuchezaji anafananishwa na nyota wa zamani wa Arsenal,Thierry Henry,limedaiwa kuwa juu kabisa ya orodha ya nyota wanaotazamwa kwa ukaribu na kocha wa Manchester City,Pep Guardiola.
Wengine ni beki wa kushoto Benjamin Mendy,22. Fabinho,23, mwenye uwezo wa kucheza beki na kiungo pamoja na kiungo Thomas Lemar,21.Hawa wote thamani yao inadaiwa kuwa ni £30m kwa kila mmoja.
Habari zaidi zinasema Manchester City itatumia mchezo wake wa marudiano wa ligi ya mabingwa Ulaya kuwatazama nyota hao kwa mara nyingine kabla ya kuingia mfukoni na kutoa pochi hiyo nene.
0 comments:
Post a Comment