Dar Es Salaam,Tanzani.
LIGI kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) inatarajiwa
kuendelea tena leo Jumapili kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja
mbalimbali nchini.
Huko Mtwara Ndanda FC watakuwa nyumbani Nangwanda Sijaona
kuwaalika African Lyon kutoka Dar Es Salaam.Mtibwa Sugar watakuwa Manungu,Turiani
kucheza na Maafande wa JKT Ruvu na huko CCM Kirumba Mwanza Mbao FC watakuwa
wenyeji wa Wanalizombe Majimaji FC kutoka Songea.
Mchezo wa mwisho leo hii utachezwa huko Chamazi,ambapo
mabingwa wa kombe la Mapinduzi Azam FC watakuwa wenyeji wa Mwadui FC kutoka
Shinyanga na mchezo huu utachezwa saa 1:00 Usiku.Michezo mingine itachezwa saa
10:00 Jioni.
Ndanda FC v African Lyon
Mtibwa Sugar v JKT Ruvu
Mbao FC v Majimaji FC
Azam FC v Mwadui FC
0 comments:
Post a Comment