728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, February 22, 2017

    Eti Obafemi Martins bado anaitaka Nigeria.

    Shanghai,China.

    MSHAMBULIAJI wa zamani wa Inter-Milan, Newcastle United na Wolfsburg,Obafemi Martins,amesema bado hajakata tamaa ya kurejea tena kuichezea timu yake ya taifa ya Nigeria licha ya kwamba hajaitwa kwenye kikosi hicho kwa kipindi cha miaka mitatu sasa.

    Martins ambaye kwa sasa anaichezea Shanghai Shenhua ya China anaamini kuwa katika umri wa miaka 32 alionao sasa bado ana mengi mazuri ya kuifanyia Nigeria kama atapewa nafasi ya kufanya hivyo na kocha wa sasa Mjerumani,Gernot Rohr.

    Martins amesema kuwa hajawahi kusema ameachana na soka la kimataifa na ikiwa Rohr atamuita basi ataupokea wito huo kwa heshima zote na kurejea kikosini.

    Nyota huyo pia amesisitiza kuwa kwa sasa yuko fiti pengine kuliko kipindi chote alichowahi kucheza soka na kuongeza kuwa kucheza kwake soka nchini China kwa sasa hakumaanishi kuwa uwezo wake umefikia ukingoni.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Eti Obafemi Martins bado anaitaka Nigeria. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top