728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, February 25, 2017

    Cristiano Ronaldo awa mwanamichezo wa kwanza kufikisha wafuasi 200m kwenye mitandao ya kijamii

    Madrid,Hispania.

    MRENO Cristiano Ronaldo ndiye mwanamichezo mwenye wafuasi wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii duniani.

    Ripoti iliyotolewa na kampuni ya HookIt inayojihusisha na kufuatilia akaunti za wanamichezo na taasisi mbalimbali imedai kuwa Ronaldo amekuwa mwanamichezo wa kwanza kufikisha wafuasi 200,000,000 kwenye mitandao ya kijamii ,Twitter, Facebook na Instagram.

    Kwa mujibu wa ripoti ya HookIt,Ronaldo ana wafuasi wengi kuliko timu zote na wachezaji wote wanaoshiriki ligi kuu nchini Marekani (MLS).Pia mara tatu zaidi ya timu zinazoshiriki ligi ya Major League Baseball ya Marekani.

    Ripoti hiyo imeendelea kupasha kuwa kila siku Ronaldo anapata wastani wa wafuasi wapya 137,000 kwenye mitandao yake ya kijamii huku nusu ya idadi hiyo ikiwa ni kwenye ukurasa wake wa Facebook ambao mpaka sasa una wafuasi 107 million.

    Nafasi ya pili inashikwa na Messi mwenye wafuasi 83.3 million.Neymar anashika nafasi ya tatu akiwa na wafuasi 21.2 million.Wayne Rooney anashika nafasi ya nne akiwa na wafuasi 12.6 million.Nafasi ya tano inashikwa na Luis Suarez mwenye wafuasi zaidi ya milioni sita.

    Kwenye mpira wa kikapu (Basketball),Lebron James ndiye kinara akiwa na wafuasi 28.2 million.Kobe Bryant yuko katika nafasi ya pili akiwa na wafuasi 8.7 million.Nafasi ya tatu imetwaliwa na gwiji wa zamani wa Chicago Bulls Michael Jordan mwenye wafuasi 2.6million.

    Kwenye Twitter,Ronaldo ana wafuasi 40.7 idadi ambayo ni mara mbili zaidi ya klabu yake ya Real Madrid yenye wafuasi 18.3million na Barcelona yenye wafuasi 16.3million.

    Kwenye Instagram, Ronaldo ana wafuasi 49.5million idadi ambayo inafuatiwa kwa karibu na Neymar mwenye wafuasi 43.4 million.Nafasi ya tatu imetwaliwa na Messi mwenye wafuasi 37.3 million.

    Hata hivyo bado Ronaldo ana kazi kubwa ya kumfikia mwanamuziki wa Marekani Taylor Swift mwenye wafuasi 71.8 million kwenye mtandao wa Twitter.67.1million Instagram na 74.2million kwenye mtandao wake wa Facebook.Idadi hiyo inamfanya Swift kuwa mbele ya Ronaldo kwa zaidi ya wafuasi 13 million.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Cristiano Ronaldo awa mwanamichezo wa kwanza kufikisha wafuasi 200m kwenye mitandao ya kijamii Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top