Zagreb,Czech.
WAKATI BEKI MTOGO,Vincent Bossou akisusa kuichezea Yanga SC kwa madai ya kutolipwa mishahara yake ya miezi minne,mwezake Francis Kone anayecheza straika wiki hii amegonga vichwa vya habari vya kimataifa baada ya kuokoa uhai wa mlinda mlango wa timu pinzani,Martin Berkovec huko Jamhuri ya Czech.
Ishu iko hivi!!Juzi Jumapili Kone,26, akiichezea timu yake ya Bohemians 1905 dhidi ya Slovacko FC kwenye mchezo wa ligi kuu ya Czech aliwahi na kumpatia huduma ya kwanza kipa wa Slovacko FC,Martin Berkovec,kwa kuuchomoa kwa kidole ulimi uliokuwa hatarini kuzama kooni hali ambayo ingepelekea apoteze uhai wa kipa huyo mwenye umri wa miaka 28.
Tukio lilikuja baada ya Berkovec kugongana na beki wake,Daniel Krch na wote kupoteza fahamu hiyo ikiwa ni katika dakika ya 29.Walipelekwa hospitalini kupatiwa matibabu zaidi.
Baada ya tukio hilo Berkovec aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook:
"Ningependa kumshukuru Francis Kone kwa jitihada zake za haraka za kuokoa uhai wangu.Niko vizuri kwa sasa,kwa mara nyingine tena nasema asante.
Akifanya mazungumzo na chombo kimoja cha habari cha Czech,Kone amesema hiyo ni mara yake ya nne anaokoa maisha ya mchezaji mwenzake.Amesema mara mbili alifanya hivyo Afrika,mara moja Thailand.
0 comments:
Post a Comment