728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, February 27, 2017

    Simba : Juuko Murshid huyu hapa


    Na Faridi Miraji.                                                  

    Yulee beki kisiki wa kimataifa wa Uganda Juuko Murishid amewasili Dar kukiongezea nguvu Kikosi cha Simba SC  kwa Mechi zilizobaki za kombe la shirikisho na zile mechi Saba za ligi kuu VPL . Juuko ambaye alikuwa na matatizo ya kifamilia kwa kufiwa na watoto wake watatu mapacha akiwa anaitumikia timu ya taifa ya Uganda kwenye michuano ya AFCON Cabon aliwasili Jana usiku.  

    Meneja wa Simba Mussa Hassan Mgossi amedhibitisha kumpokea Juuko na kumwambia awasili jumatatu kwenye mazoezi ya timu hiyo uwanja wa Polisi baada ya wachezaji wote wa Simba kupewa mapumziko ya siku moja jana. Kurudi Kwa Juuko kunaweza kuwa faraja Kwa wanachama na wapenz wa Simba kutokana na beki wao Method Mwajale kuwa majeruhi na Bado hawana imani na beki Novart Lufunga. 

    Mpango wa Kumrejesha Juuko ulianzia Zanzibar kwenye kambi ya kujiandaa na mchezo wa watani wa jadi uliochezwa Jana na Simba kushinda Kwa magoli mawili Kwa moja la Yanga.  Viongozi wa Simba walianza harakati za kumuwahisha Juuko ili kuwahi mechi ya watani kutokana na Mwajale kutokuwa na utimamu wa Mwili.  Jambo ambalo Bechi la ufundi walilipinga Kwa kuhofia kushusha morali ya wachezaji. 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Simba : Juuko Murshid huyu hapa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top