London,England.
HARRY Kane akipongezwa na wachezaji wenzake wa Tottenham baada ya kufunga mabao matatu (hat-trick) katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stoke City katika mchezo wa ligi kuu England uliochezwa jioni ya leo huko White Hart Lane .
Kane,23,amefunga mabao hayo katika dakika za 14,32 na 37 na kumfanya nyota huyo wa England afikishe mabao 17 sawa na Alexis
Sanchez na Romelu Lukaku.Bao la nne limefungwa na Delle Alli katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza.
Aidha hat-trick hiyo imemfanya Kane afikishe hat-trick tatu katika michezo tisa iliyopita.Pia akifikisha mabao 100 akiwa na Tottenham.
Vikosi
Stoke XI vs. Spurs: Grant;
Bardsley, Shawcross, Martins Indi, Pieters; Whelan, Adam;Arnautovic, Allen, Ramadan;Crouch.
Spurs XI vs. Stoke: Lloris; Dier,Alderweireld,Vertonghen; Walker,
Wanyama, Dembele, Davies; Eriksen,Alli; Kane.
0 comments:
Post a Comment