Sevilla,Hispania.
SAMIR Nasri amemtetea kocha wake wa zamani Arsene Wenger na kudai kuwa wanaoikwamisha Arsenal kutwaa vikombe ni wachezaji pamoja na wakurugenzi wa bodi ya klabu hiyo.
Nasri ambaye kwasasa yuko Sevilla ya Hispania akitokea Manchester City kwa mkopo amesema wachezaji wa Arsenal ndiyo wanaopaswa kuwajibika katika kipindi hiki ambacho klabu yao inapata matokeo mabaya.
Akifanya mahojiano na kituo cha Sky Sports,Nasri amesema siyo haki kumtupia lawama zote Wenger wakati wanaoikwamisha Arsenal ni wachezaji ambao wameshindwa kupata matokeo mazuri uwanjani.
"Sidhani kama tatizo ni Wenger.Kuna wachezaji,kuna bodi - kuna mambo mengi sana yanayoendelea klabuni Arsenal.Amesema Nasri aliyeihama Arsenal mwaka 2011.
0 comments:
Post a Comment