Na Faridi Miraji.
Beki wa kimataifa wa Togo Vicent Bossue alikuwa anaiwakilisha timu yake ya taifa kwenye michuano ya AFCON huko Gabon alivyorudi alikuta timu Iko kwenye Maandalizi ya mechi dhidi ya Ngaya club ya Cammoro alifanya mazoezi na timu lakini hakujumuishwa timu iliyosafiri kwenda Commoro. Yanga wakaenda kumaliza shughuli huko Commoro Kwa kuwafunga magoli matano Kwa moja tena kwao wakarahisisha mechi ya marudiano ambapo Bossue akajumuishwa kwenye program ili awe fiti kuelekea mechi ya watani iliyochezwa juzi.
Baaada ya mechi ya marudiano dhidi ya Ngaya club., Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Vodacom wakaenda kuweka kambi kimbiji huko Kigamboni wakiwa na Vicente Bossue alikuwa kwenye mipango ya Mwalimu ila dakika za mwisho siku moja kabla ya Pambano Bossue akakolofishana na kamati ya hamasa Kwa kuwakumbushia ahadi yake ya malipo ambayo walimuahidi atalipwa . wakati Akiwa kwenye AFCON Bossue hakuona chochote kwenye account yake alivyorudi aliuliza uongozi Ukawa unampiga Danadana.
Baadae aliongea na baadhi ya wachezaji wakampa mbinu namna ya kushungulikiwa matatizo yake na jibu alilopewa ni mechi dhidi ya Simba ndio maana Bossue alishinikiza uongozi umutatulie matatizo yake mapema kabla ya mechi dhidi ya Simba lakini hawakufikia mwafaka mpaka akaondolewa kwenye mipango ya Mwalimu dakika za mwisho.
Uongozi wa Yanga umesema hauna tatizo na mchezaji huyo na wanashidwa kumuelewa . Na kuhisi Kama anatumiwa na wapinzani kuiua Yanga kiongoz mmoja alisema kwanza tumemvumilia Sana Bossue Alikuwa anajenga makundi ndani ya wachezaji aliendaga ulaya kuongea na timu akasema anunue mkataba wake yakamshinda tukamupokea Kwa mikono mawili na alishavunja masharti ya mkataba ila tukamsamehe ila yeye haoni. timefungwa na Simba ikiwa pungufu wachezaji hawana Morali tuna mechi dhidi ya Ruvu Kesho kutwa unategemea nini liwalo na liwe tu.
Kumekuwa na mkanganyiko juu ya wachezaji wa kulipwa na Uongozi baada ya Ngoma kurumbana na uongozi kuhusu kuumwa kwake daktar wa timu anasema amepona limebaki jukumu la kocha kumtumia au lakini yeye akaja na daktar wake akasema Bado hajapona mkanganyiko ukaibuka. Mmoja wa mashabiki wa kutupwa wa Yanga alisema hata Ngoma angekuwa anaumwa angeenda kambini tu ili kuongeza Morali Kwa wachezaji wake Mbona Simba Wamemupeleka Mwanjale Huku wakijua anaumwa ili kuwajenga kisaikolojia wachezaji. Na ndio maana alivyokosekana Mwanjale wachezaji wetu wakawadhalau simba. Ndio hivyooo hivyooo hata sisi tungefanya Ila uongozi unaongea tu.
Siku za Vicente Bossue zinahesabika ndani ya Yanga Leo kutakiwa na kikao ila inakuwa ni siri Sana kikao hicho ni cha kuweka mambo Sawa kuelekea mechi zao dhidi Ruvu shooting na mechi ya kimataifa dhidi ya Zanaco March 11, na suala la Bossue litajadiliwa pamoja na mechi ya Simba. kuna asilimia kubwa Yanga kuachana na Bossue hata kabla ya kumalizika kwa mkataba wake mwishoni mwa msimu.
0 comments:
Post a Comment