728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, February 22, 2017

    Waganda wazidi kutoboa soka la kimataifa

    Kampala,Uganda.

    WAKATI Tanzania tukijivunia Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kama wachezaji pekee wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya,wenzetu Uganda wameendelea kutoboa soka la kimataifa siku hadi siku kwa nyota wao wengi kuendelea kupata nafasi za kucheza soka karibu kila pande za dunia. 

    Jana Jumanne kiungo wa kimataifa wa Uganda,Khalid Aucho aliripotiwa kujiunga na mabingwa wa zamani wa Ulaya Red Star Belgrade ya Serbia kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu.

    Aucho,23,ambaye siku chache zilizopita yeye pamoja na nahodha wa Uganda,Geofrey Massa walitupiwa virago na Baroka FC ya Afrika Kusini amepata shavu hilo baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye michuano ya AFCON iliyofanyika nchini Gabon hivi karibuni.

    Wakala Mserbia Ivica Stankovic,ambaye pia ni wakala wa kipa wa Mamelodi Sundown,Denis Onyango,amedaiwa kuwa ndiye aliyefanikisha uhamisho huo wa Aucho.

    Kwa sasa Red Star Belgrade wanaongoza ligi kuu ya Serbia wakiwa na alama 57 katika michezo 22,alama sita juu ya wapinzania wao wa jadi Partizan Belgrade.

    Ikiwa Red Star Belgrade watatwaa ubingwa msimu huu watapata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu wa 2017/2018. 

    Lakini kwa kuanzia Aucho atajiunga na klabu ya OFK Beograd ya daraja la kwanza kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita ili kupata uzoefu wa kucheza soka Ulaya.

    Kwa sasa Aucho yuko nchini kwao Uganda akisubiria kukamilika kwa hati yake ya kusafiria (VISA) kabla ya wikendi hii kuelekea  nchini Serbia kuanza maisha mapya katika mji wa Belgrade.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Waganda wazidi kutoboa soka la kimataifa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top