728x90 AdSpace

Sunday, February 19, 2017

Balotelli anyukwa kadi nyekundu ya tatu Ufaransa,Nice ikishinda ugenini

Lorient,Ufaransa.

MARIO Balotelli ameendelea kuudhihirishia Ulimwengu kuwa si mchezaji anayejitambua hata kidogo hii ni baada ya jana Jumamosi kunyukwa kadi nyekundu ya tatu tangu atue Ufaransa mwezi Agosti mwaka jana kuichezea OGC Nice.

Balotelli,26,alitolewa uwanjani katika dakika ya 68 kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kufuatia kumfanyia madhambi beki wa Lorient,Zargo Toure na kisha kumkoromea mwamuzi wa mchezo huo,Tony Chapron.


Hiyo inakuwa kadi nyekundu ya tatu kwa Balotelli katika kipindi kisichozidi miezi sita.Kadi ya kwanza ilikuwa dhidi ya Lorient mwezi Octoba na ya pili mwezi Disemba dhidi ya Bordeaux.

Kadi nyingi nyekundu ugenini kuliko mabao!!

Mpaka sasa Balotelli ameifungia Nice mabao tisa,yote akiyafunga kwenye uwanja wa nyumbani.Hajafunga bao lolote ugenini,kaambulia kadi mbili nyekundu,moja nyumbani.

Nice yashinda Ugenini

Licha ya kucheza pungufu, Nice imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Wylan Cyprien katika dakika ya 15 baada ya kazi nzuri ya Arnaud Souquet.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Balotelli anyukwa kadi nyekundu ya tatu Ufaransa,Nice ikishinda ugenini Rating: 5 Reviewed By: Unknown